Atilano

Picha yake.

Atilano (Tarazona, 850 - Zamora, 5 Oktoba 919 hivi) alikuwa askofu wa kwanza wa Zamora, nchini Hispania, kuanzia mwaka 901 hadi 917.

Kabla ya hapo alikuwa mkaapweke na mmisionari pamoja na Froilano katika maeneo ambayo Wakristo waliyakomboa kutoka mikononi mwa Waislamu [1].

Tangu zamani anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 5 Oktoba[2].

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/73060
  2. Martyrologium Romanum

Developed by StudentB