Kihaji ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Wahaji kwenye kisiwa cha Sumatra. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kihaji imehesabiwa kuwa watu 17,500. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kihaji iko katika kundi la Kimalayiki. Takriban asilimia 30 za msamiati wa Kihaji ni maneno makopo kutoka Kilampung.