Kimok ni lugha ya Kiaustro-Asiatiki nchini Uthai inayozungumzwa na Wamok. Mwaka wa 1981 idadi ya wasemaji wa Kimok imehesabiwa kuwa watu saba tu, yaani inawezekana kwamba lugha imeshatoweka kabisa sasa. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kimok iko katika kundi la Kipalaungiki.