Kisa'a ni lugha ya Kiaustronesia nchini Visiwa vya Solomon inayozungumzwa na Wasa'a kwenye visiwa vya Ulawa na Malaita. Mwaka wa 1999 idadi ya wasemaji wa Kisa'a imehesabiwa kuwa watu 11,500. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kisa'a iko katika kundi la Kioseaniki.