Albert Einstein (14 Machi 1879 – 18 Aprili 1955) alikuwa mwanafizikia mwenye asili ya Kiyahudi kutoka nchi ya Ujerumani. Hasa anajulikana kwa nadharia ya uhusianifu. Mwaka 1921 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia. Mwaka 1933 alipoona kuwa Hitler aliteka utawala nchini Ujerumani, aliamua kubaki Marekani alipokuwa amekwenda, na hatimaye alipata uraia wa huko mwaka 1940.