Ago - Septemba - Okt | ||||||
1 | 2 | 3 | 4 | 5 | 6 | 7 |
8 | 9 | 10 | 11 | 12 | 13 | 14 |
15 | 16 | 17 | 18 | 19 | 20 | 21 |
22 | 23 | 24 | 25 | 26 | 27 | 28 |
29 | 30 | |||||
Kalenda ya Gregori |
Tarehe 23 Septemba ni siku ya 266 ya mwaka (ya 267 katika miaka mirefu). Mpaka uishe zinabaki siku 99. Kwa kawaida ama ni sikusare otomnia ya kaskazini au siku ya kwanza baada ya sikusare hiyo. Katika nusutufe ya kaskazini ya dunia mchana huanza kuwa mfupi na muda wa usiku kuwa mrefu zaidi kuliko mchana. Kwenye nusutufe ya kusini mwendo ni kinyume: kuanzia sasa mchana hurefuka na giza la usiku kupungua. Mabadiliko hayo yanaonekana kote duniani kwenye umbali fulani kutoka ikweta.