Anatomia (pia anatomi[1], en:anatomy, kutoka Kigiriki ἀνατέμνειν anatemnein - kupasua, kufungua) ni elimu ya miili ya viumbehai kama binadamu, wanyama na mimea. Inachungulia muundo na umbile la mwili na sehemu au viungo vyake.
Wataalamu wa anatomia hufungua mwili na kuikata kwa sehemu zake kwa kusudi la kuongeza elimu ya muundo wake.
Elimu hii inasaidia kuelewa magonjwa, pamoja na sababu na matokeo yake. Ni pia msingi wa mafundisho ya tiba na elimu ya matibabu.