Ario (kwa Kiberberi: Aryus ; kwa Kigiriki Ἄρειος, Areios, 250 au 256 – 336) alikuwa padri kutoka Libya aliyefanya kazi huko Alexandria, Misri.[1]
Mafundisho yake[2][3] yalisisitiza kuwa Mungu Baba ni mkuu kuliko Mwana,[4] akipinga imani katika Utatu.[5]
Kristolojia yake ilikanushwa na askofu wake, Aleksanda wa Aleksandria, lakini ilienea kote mashariki mwa Dola la Roma na kuvuruga Kanisa Katoliki kiasi cha kudai Kaisari Konstantino I aitishe Mtaguso wa kwanza wa Nisea mwaka 325.
Huo mtaguso mkuu wa kwanza, uliokusanya maaskofu wengi hasa wa mashariki, ulikataa hoja zake na kumkiri Mwana kuwa na hali ileile ya Baba.
Hata hivyo vurugu ziliendelea hata kudai ufanyike mtaguso wa kwanza wa Konstantinopoli (383), ambao ni wa pili kati ya mitaguso ya kiekumene, nao ukasisitiza na kukamilisha imani ya mtaguso wa kwanza wa Nisea katika Kanuni ya Imani ya Nisea-Konstantinopoli.
Ingawa imani hiyo ilikubaliwa kura rasmi katika Dola la Roma, Uario ulienea kati ya makabila ya Kijerumani, hasa Wagoti na Wavandali, hivyo uliendelea hadi karne ya 7 na ya 8.
Mpaka leo kuna madhehebu yanayokanusha umungu wa Yesu Kristo na kusema ni kiumbe tu.
Arius, who was born in Libya, was a respected ascetic and presbyter at the church of the Baucalis in Alexandria.