Asilimia (kutoka maneno mawili ya Kiarabu اصل asl yaani asili, chanzo na مئوية mia 100 ) ni njia ya kutaja uhusiano kati ya idadi mbili tofauti. Alama yake ni %. Kiasi kimoja huteuliwa kuwa ni namba ya 100 ya kiasi kingine. Sehemu yake ya mia ni 1 %.
Sasa inawezekana kugawa kiasi kingine kwa ile 1% na kuona inashika asilimia ngapi za kiasi husianifu.