Daraja

Daraja juu ya mto huko Hispania.

Daraja ni jengo lililoundwa kwa kusudi la kuwa na njia ya kupitia juu ya pengo au kizuizi. Mfano mzuri ni daraja linaloendeleza barabara juu ya mto, bopo au juu ya barabara nyingine.

Kuna aina nyingi za madaraja. Ukubwa wa daraja unategemea upande mmoja upana wa kizuizi kinachotakiwa kuvukiwa, yaani upana wa mto au bopo, na kwa upande mwingine uzito wa mizigo itakayopita juu ya daraja. Daraja la kuvukisha watu halina mzigo mkubwa lakini daraja linalopokea njia ya reli au barabara kuu litabeba uzito mkubwa.

Kuna pia madaraja yanayovusha mfereji juu ya mto hivyo kuwezesha meli kupita juu ya meli nyingine. Kwa jumla madaraja ni sehemu muhimu za miundombinu ya kila nchi.

Upande wa kusini wa daraja la Lake Pontchartrain

Developed by StudentB