Dawa (kwa Kiingereza drug) ni dutu lolote -kama si chakula- ambalo linabadilisha hali ya mwili au ya roho ya mtu baada ya kuingizwa mwilini mwake.
Njia za kuingiza dawa mwilini ni pamoja na mdomo, pua, ngozi au sindano.
Kuna madawa asilia yanayoundwa kutokana na mimea na mengine sintetiki (yaani yaliyotengenezwa kwa njia ya kikemia).
Mara nyingi dawa hutumiwa na binadamu kwa makusudi. Yanamezwa, kupakiwa au kudungwa kwa sindano. Kuna pia madawa yanayoweza kuathiri watu yakiwafikia bila kukusudi, mfano kwa kuliwa bila kujua au kutokana na usambazaji wa dawa hewani au kwenye maji kwa mfano baada ya moto mkubwa au ajali.