Duara ni umbo la mviringo bapa yaani katika ubapa linalofanana na herufi "o".
Katika jiometria duara huelezwa kuwa mchirizo uliofungwa na umbali wa kila nukta ya mchirizo ni sawa kutoka kitovu cha duara.
Mstari wa nje wa duara huitwa mzingo. Katikati yake ni kitovu. Mstari usioonyoka kutoka kitovu hadi mzingo huitwa rediasi au nusukipenyo. Mstari wowote kutoka upande mmoja wa mzingo hadi upande mwingine unaopita kwenye kitovu huitwa kipenyo.
Kiwango cha kipenyo (d) ni mara mbili kiwango cha nusukipenyo (r).
Katika mahesabu ya duara namba inayoandikwa kwa herufi ya kigiriki π (tamka: pi) ni muhimu. Ni sawa na urefu wa mzingo (c) uliogawiwa kwa urefu wa kipenyo na ni takriban 3.14159.
Eneo la duara (a) ni sawa na zao ya nusukipenyo (r) mara nusukipenyo halafu mara π (a ni π mara (r mara r)).