Encyclopædia Britannica ni kamusi elezo kubwa na moja kati ya kamusi elezo iliyo-maarufu zaidi. Inaandikwa kwa lugha ya Kiingereza. Kamusi elezo hii huchapishwa na kampuni binafsi ya Encyclopaedia Britannica, Inc. Awali ilikuwa ikichapishwa kwenye karatasi tu, lakini hivi karibuni imepanuka na kuwa na dijiti, au matoleo ya kompyuta vilevile. Kamusi elezo hii imegawanyika katika vitabu vingi sana. Makala za kwenye vitabu zimepangwa kwa mtindo wa kialfabeti. Kumekuwa na matoleo yake ambayo ni kwa ajili ya watoto vilevile. Hii ni kamusi elezo kubwa sana ya kuchapishwa. Kamusi elezo iliyo-kubwa ziadi ni Wikipedia. Watu wengi huhesabia kwamba ni kamusi elezo bora, kwa sababu ipo sahihi na ina mambo mengi.
Kamusi elezo hii awali ilikuwa ndogo sana, toleo la kwanza lilikuwa na vitabu vitatu na ilitolewa mnamo mwaka wa 1768. Polepole likawa kubwa zaidi. Toleo jipya, toleo la 15, sasa lina vitabu takriban 29, jumlisha vitabu viwili ambavyo ni faharasa. Pia imemjulisha kitabu cha ziada kiitwacho Propaedia, kwa ajili ya kuainisha ufahamu. Vitabu 29 vimeumba Macropaedia na Micropaedia. Macropædia ni kikubwa kuliko vingine, chenye makala yenye maelezo zaidi ambazo pia zaweza kuwa na kurasa 300, -metengenezwa kwa vitabu 17, wakati Micropædia ni kidogo ambacho kawaida huwa na makala fupi na maneno machache chini ya 750. Micropædia hutumika kwa ajili ya kutazama kwa haraka zaidi, lakini iwapo utahitaji habari zaidi basi inakubidi utumie Macropædia. Kila kitabu kimoja ni kikubwa sana, zaidi ya kurasa 1,000 kwa kitabu. Kuna vitabu vya mwaka. Kila mwaka, kitabu kimechapishwa kuhusu matukio ya mwaka huo.
Makala za kwenye Britannica ni kwa ajili ya watu wazima walio-elimika, si kwa ajili ya watoto, na imeandikwa na wahariri takriban 100 na wachangiaji wataalamu zaidi ya 4,000. Watu wengi hudhania ni kamusi elezo bora, lakini Wikipedia bado inabaki kuwa maarufu kwa kuwa matumizi yake ni bure. Britannica ni kamusi elezo ya kale kwa lugha ya Kiingereza mpaka sasa. Ilianza kuchapishwa kwa mara ya kwanza kunako mwaka kati ya 1768 na 1771 huko mjini Edinburgh, Uskoti na kukua kwa umaarufu mkubwa, ikiwa na toleo lake la tatu mnamo 1801 ikiwa imeongeza vitabu 21.
Ukubwa wa vitabu vya Britannica karibia vyote vinafanana kwa takriban miaka 70, ikiwa na maneno yapatayo milioni 40 ikiwa ni nusu ya mada zilizopo ndani ya vitabu vyenyewe. Kamusi elezo hii awali ilikuwa ikimilikiwa na Uingereza. Kwa sasa inamilikiwa na Marekani, lakini bado inaandikwa kwa Kiingereza cha Uingereza. Muda wa ziada, kamusi elezo hii imekuwa na kipindi kigumu cha upatikanaji wa fedha, kitu ambacho kamusi elezo nyingi huzikumba.