Farakano la mwaka 1054 lilitokea hasa kati ya Papa Leo IX wa Roma na Patriarki Mikaeli Serulari wa Konstantinopoli likasababisha ushirika kati ya Ukristo wa Magharibi na sehemu kubwa ya Ukristo wa Mashariki usiendelee kuwa kamili hadi leo.
Mahusiano yalikuwa yamezidi kuharibika tangu karne ya 4 ambapo ulianza ushindani kati ya miji hiyo miwili iliyokuwa kwa pamoja makao makuu ya Dola la Roma.
Maelekeo tofauti katika teolojia, maisha ya kiroho n.k. yalitumika kama visingizio katika kulaumiana, na hata kufarakana kwa muda.[1][2][3][4][5]
Hatimaye mabalozi waliotumwa na Papa, ingawa hawakuwa na mamlaka hiyo, waliacha juu ya altare ya kanisa kuu la Konstantinopoli hati ya kumtenga Patriarki na Kanisa Katoliki, naye akaitikia kwa kumtenga Papa na Kanisa la Orthodoksi.
Juhudi mbalimbali za kurudisha umoja zilifanyika katika nafasi mbalimbali, lakini pengine haraka haikusaidia kuzifanikisha, kwa mfano katika Mtaguso wa pili wa Lyon (1274) na katika Mtaguso wa Firenze (1431-1449).
Njia ya taratibu iliyoshikwa pamoja katika karne ya 20 inatia tumaini zaidi. Inakumbukwa hasa tamko la upendo la tarehe 7 Desemba 1965 ambalo Papa Paulo VI na Patriarki Atenagora I kwa pamoja walifuta kutoka kumbukumbu ya Kanisa hati za mwaka 1054 ambazo pande hizo mbili zilitengana.
{{citation}}
: Unknown parameter |trans_title=
ignored (|trans-title=
suggested) (help).
{{citation}}
: CS1 maint: location missing publisher (link) CS1 maint: unrecognized language (link).
{{citation}}
: CS1 maint: location missing publisher (link) CS1 maint: unrecognized language (link).
{{citation}}
: CS1 maint: location missing publisher (link) CS1 maint: unrecognized language (link).