Ghala ni jengo linalohifadhi bidhaa kama vile malighafi, vipuri, au bidhaa zinazohusiana na kilimo, viwanda na uzalishaji.
Ghala hutumiwa na wazalishaji, waagizaji, wauzaji wa nje, wauzaji wa jumla, wafanya biashara za usafiri, forodha, n.k.
Kwa kawaida huwa majengo makuu makubwa katika maeneo ya viwanda ya mijini na vijijini.
Mara nyingi huwa na sehemu maalum ya kupakia na kupakua bidhaa kutoka kwenye malori. Wakati mwingine ghala hujengwa kwa ajili ya upakiaji na upakuaji bidhaa wa moja kwa moja kutoka kwenye reli, viwanja vya ndege, au bandari.
Mara nyingi huwa na kambarau kwa ajili ya kunyanyua bidhaa.