Ghuba ya Guinea ni kidaka kikubwa cha bahari ya Atlantiki kwenye pwani ya magharibi mwa Afrika.
Eneo lake linahesabiwa kuanza nchini Liberia kwenye rasi ya Palmas na kwisha kwenye rasi Lopez nchini Gabon.
Jina la "Guinea" limetokana na jina la kale la sehemu kubwa ya upande wa kusini wa Afrika ya Magharibi kati ya jangwa la Sahara na Atlantiki likimaanisha "nchi ya watu weusi" kwa lugha ya Kiberber.
Kati ya mito mikubwa inayoishia kwenye ghuba hiyo ni Niger, Volta na Kongo.
Mwambao wa ghuba una vidaka viwili vidogo ambavyo ni hori ya Benin na hori ya Biafra (Nigeria imebadilisha jina hili kuwa hori ya Bonny baada ya vita vya Biafra).