Hisabati ni somo linalohusika na idadi, upimaji na ukubwa wa vitu.
Kwa ujumla linahusika na miundo na vielezo.
Hisabati linaundwa na masomo mbalimbali, kama hesabu, jiometria na aljebra.
Neno hisabati katika lugha ya Kiswahili limetokana na neno la Kiarabu حسابات (halisi: hesabu (wingi)).
Somo hili huweza kutumika kutatua matatizo mbalimbali, lakini hasa ni la msingi katika uelewa wa ulimwengu kisayansi. Hivyo hutumiwa na masomo mengine kama Fizikia, Jiografia, Kemia katika mafunzo yake.