Sehemu ya mfululizo wa makala juu ya |
Imani na ibada zake |
Umoja wa Mungu |
Waislamu muhimu |
Abu Bakr • Ali |
Maandiko na Sheria |
Qur'an • Sunnah • Hadithi |
Historia ya Uislamu |
Historia |
Tamaduni za Kiislamu |
Shule • Madrasa |
Tazama pia |
Historia ya Uislamu kadiri ya wafuasi wa dini hiyo haikuanza na Mtume Muhammad kama wanavyofikiria watu wengi bali imeanza tangu alipoletwa nabii wa kwanza ulimwenguni, ambaye kwa mujibu wa Waislamu ni Nabii Adamu alipoteremshwa ulimwenguni na kupewa mwongozo na Mwenyezi Mungu wa namna gani kuishi hapa duniani kwa njia nzuri ya wema na hisani kwa kushikamana na mafunzo yake Mwenyezi Mungu na kujiepusha na makatazo yake.
Masimulizi ya historia hii ya Uislamu yameelezwa katika vitabu vitakatifu vya Mitume mbali mbali waliokuja duniani na kadhalika katika Qurani Tukufu. Umma mbali mbali zilizopita huko nyuma zimetajwa katika Qurani na kuelezwa namna gani zilivyoangamizwa kwa kutokubali ujumbe wa Mwenyezi Mungu na kuwakataa Mitume yake nao wakaletewa adhabu kali ya upepo au mvua au mafuriko na kadhalika.
Inasemekana katika historia ya Uislamu kuwa Mwenyezi Mungu alileta Mitume na Manabii kiasi cha 124,000 kwa ajili ya kuwaongoza binadamu kutokana na giza la ujinga na ujahili na utumwa wa kuabudu miungu mingi kuwatia kwenye nuru na mwangaza wa elimu na maarifa na ujuzi wa kumjua Mwenyezi Mungu wao aliyewaumba na kuwafanya wawakilishi wake hapa duniani. Mitume hawa na Manabii waliletwa na Mola wao kuwafahamisha wanadamu ukweli na haki iko wapi na wengine katika wao wakapewa vitabu ili wawaongoze wenziwao katika wanadamu kuwaelekeza kwenye njia ya haki.
Visa vya Mitume na Manabii hawa vinatueleza mengi kuhusu hawa wajumbe watukufu wa Mwenyezi Mungu na kuwa wote walitumwa na Mola wao kutangaza Umoja na Upweke wa Mwenyezi Mungu na kuwa Yeye hana mshirika na pekee ndiye mwenye kustahiki kuabudiwa kwa haki asishirikishwe na chochote au yeyote katika viumbe vyake wakiwa ni binadamu wenziwao au mizimu au majini au wanyama au vyenginevyo katika viumbe vyake.