Ibada

Sehemu ya mchoro Dini wa Charles Sprague Pearce (1896).

Ibada ni tendo la heshima ya hali ya juu linalotolewa kwa Mwenyezi Mungu au kwa chochote kile kinachoheshimiwa kama mungu.

Inaweza kufanywa na mtu binafsi au na kundi, hasa likiongozwa na kuhani au mwingine aliyekubalika.

Dini zinaelekeza binadamu kufanya ibada inavyotakiwa.

Ibada inasisitiza ukweli wa yule anayetolewa heshima hiyo, kwa mfano kutokana na imani ya dini fulani.[1] Vilevile ukweli wa mtoaji kwa maana ibada lazima itoke moyoni: ndiyo sababu haiwezi kulazimishwa.

Neno la Kiswahili linatokana moja kwa moja na Kiarabu ambapo neno عبادة, ibadah, linahusiana na maneno mengine kama vile "utumwa", na linadokeza utiifu na unyenyekevu hasa kwa Mungu pekee, inavyodaiwa na Uyahudi, Ukristo na Uislamu.[2]

Ukristo unasisitiza umuhimu wa kumuabudu Mungu kama Baba kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu na kufuata ukweli uliofundishwa na Yesu Kristo.

Uislamu unaona ibada kuwa lengo lenyewe la uumbaji wa binadamu na majini.[3][4] Katika karne ya 13 mwanachuo Ibn Taymiyyah aliieleza ibada ni "neno pana linalojumlisha kila jambo ambalo Allah analipenda na anapendezwa nalo - lile usemi au matendo, ya nje na ya ndani".[5][6]

Wataalamu wa sosholojia wanaonyesha kwamba wasio na dini wanaweza wakaabudu mambo mengine kama vile timu ya mpira, chama cha siasa, taifa au wasanii mbalimbali.[7][8]

Katika Kiswahili neno linaweza kuwa na maana ya mazoea: "Kwake ulevi ni ibada".

  1. Nagata, Judith (Juni 2001). "Beyond Theology: Toward an Anthropology of "Fundamentalism"". American Anthropologist. 103 (2).{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. al-Qamoos al-Muhit
  3. "Al-Qur'an 51:56".
  4. Kuhusu swalah tano, Mtume aliripotiwa kusema, Swalini kama munavoniona mimi nikiswali [Imepokewa na Bukhari] Aisha alipokewa kwamba alisema: (Mtume alikuwa akifungua Swalah kwa Takbiri na kisomo cha “Alhamdu lillaahi Rabbil ‘aalamiin”, na alikuwa akirukuu hakiinamisha kichwa chake na wala hakisimamishi sawa, bali alikiweka baina ya hali hizo mbili. Na alikuwa akiinua kichwa chake kutoka kwenye rukuu, hasujudu mpaka alingane katika kusimama. Na alikuwa akisoma Atahiyatu katika kila rakaa mbili, na alikuwa akikalia mguu wake wa kushoto na akiusimamisha mguu wake wa kulia. Na alikuwa akikataza mkao wa Shetani (kukaa kama shetani) na alikikataza mtu kuiweka chini mikono yake katika kukaa kama vile mnyama wa kuwinda, na alikuwa akihitimisha Swala yake kwa kupiga Salamu) [Imepokewa na Muslim.]
  5. Majmu' al-Fatawa (10/149)
  6. https://www.al-feqh.com/sw/namna-ya-kuswali
  7. http://sydney.edu.au/news/84.html?newsstoryid=10384
  8. http://www.cf.ac.uk/socsi/undergraduate/introsoc/durkheim6.html

Developed by StudentB