Imamu (kutoka Kiarabu: إمام imām) ni istilahi ya Kiarabu yenye maana mbalimbali. Mara nyingi inamtaja kiongozi wa Kiislam, kama kiongozi wa msikiti au wa jamii. Maana ya msingi ni yule anayetoa mwongozo akistahili kufuatwa; kwa maana isiyo ya kidini neno hili linaweza kutaja pia timazi au kamba inayotumiwa kuelekeza mwendo wa matofali wakati wa kujenga nyumba au ukuta.[1]
Imamu anaitwa yule anayeongoza sala wakati wa swala ya Kiislamu.