Imani sahihi

Kanuni ya Imani ya Nisea ni kigezo kimojawapo cha kupimia usahihi wa imani katika Ukristo.

Imani sahihi (kwa Kiingereza Orthodoxy, kutoka maneno ya Kigiriki orthos + doxa,[1]) ni msimamo unaokubali mafundisho sanifu ya dini fulani, tofauti na yale ya wachache.[2]

Umuhimu wa jambo hilo unasisitizwa hasa katika dini inayokiri umoja wa Mungu, lakini si katika dini nyingine kama zile za jadi au za miungu mingi.

Katika Ukristo, inamaanisha kwa kawaida kukubali imani kama ilivyofundishwa na mitaguso ya kiekumene katika karne za kwanza za dini hiyo dhidi ya uzushi wa aina mbalimbali.[1]

  1. 1.0 1.1 orthodox. Dictionary.com. Online Etymology Dictionary. Douglas Harper, Historian. Dictionary Definition (accessed: March 03, 2008).
  2. orthodox. Dictionary.com. The American Heritage Dictionary of the English Language, Fourth Edition. Houghton Mifflin Company, 2004. Dictionary definition (accessed: March 03, 2008).

Developed by StudentB