Injili ya Mathayo

Ukurasa wa kwanza wa Injili ya Mathayo ulichorwa mnamo mwaka 1240 Ulaya ukionyesha mamajusi watatu mbele ya mtoto Yesu.
Mchoro huu kutoka Ufaransa (mnamo mwaka 800) wamuonyesha Mwinjili Mathayo akipokea maneno ya Injili yake kutoka kwa malaika.
Agano Jipya

Injili ya Mathayo ni kitabu cha kwanza katika orodha ya vitabu vya Agano Jipya katika Biblia ya Kikristo.

Huhesabiwa kati ya Injili Ndugu pamoja na Marko na Luka, kwa sababu inafanana nazo kwa kiasi kikubwa; hasa inatumia asilimia 80 ya maandiko ya mwinjili Marko.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.


Developed by StudentB