Inosenti wa Imakulata, C.P. (jina la kuzaliwa: Manuel Canoura Arnau; Foz, Lugo, 10 Machi 1887 – Turon, 9 Oktoba 1934) alikuwa padri Mpasionisti wa Hispania[1] aliyeuawa na waasi wa dini bila kesi kwa ajili ya imani yake, akiwa pamoja na mabradha 8 wa shirika la Mabradha wa Shule za Kikristo: Sirili Bertran, Marchano Yosefu, Viktoriano Pio, Benjamini Juliani, Juliani Alfredo, Augusto Andrea, Benito wa Yesu na Aniseto Adolfo[2][3].
Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri tarehe 19 Aprili 1990, halafu mtakatifu tarehe 21 Novemba 1999 pamoja na wafiadini wenzake.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifodini chake[4].