Itifaki (kutoka neno la Kiarabu; pia "protokali", kutoka Kiingereza "protocol") ni orodha au mpangilio wa visa unaotumika katika kuendesha sherehe, mkutano, mjadala na kadhalika kutokana na utaratibu uliowekwa. Mathalani katika shughuli za mikutano ni kiongozi gani anatakiwa kuingia kwanza, kisha nani afuatie na nani awe wa mwisho kuingia katika sehemu ya mkutano. Mwenyeji wa mkutano anatakiwa kukaa upande gani na mgeni mwalikwa anatakiwa kukaa upande gani. Kama ni shughuli ya kitaifa ni wimbo wa taifa gani unatakiwa uanze, ule wa Rais mwenyeji au wa Rais mgeni? Baada ya mkutano nani anatakiwa kutoka kwanza na nani awe wa mwisho. Mambo kama haya au utaratibu kama huu ndio huitwa itifaki. Ila mwanafunzi afahamu kwamba itifaki ikitumika katika isimujamii inaleta dhana tofauti na maelezo haya.
Pia ni maelewano au maridhiano maalumu kati ya mataifa.
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Itifaki kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |