Jamhuri inataja aina za serikali zisizo na mfalme, malkia, sultani au mtemi wowote.
Mara nyingi wananchi humchagua kiongozi wao akiitwa mara nyingi rais. Kuna pia vyeo vingine.
Katika nadharia jamhuri inatakiwa kufuata muundo wa demokrasia. Lakini kuna pia jamhuri pasipo na serikali inayochaguliwa zikifuata kwa mfano muundo wa udikteta au utawala wa kijeshi.
Kinyume chake kuna pia muundo wa ufalme pamoja na demokrasia, kwa mfano Uingereza au Uswidi.
Makala hii kuhusu mambo ya siasa bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |