| |||||
Kaulimbiu ya taifa: | |||||
Wimbo wa taifa: Maandamano ya wale wanaojitolea - ''Yìyǒngjūn Jìnxíngqǔ'' | |||||
Mji mkuu | Beijing | ||||
Mji mkubwa nchini | Shanghai | ||||
Lugha rasmi | Kimandarini1 (Putonghua) | ||||
Serikali | Ujamaa jamhuri ya chama kimoja2 Xi Jinping Li Keqiang | ||||
Tarehe za kihistoria Utawala wa nasaba ya Shang Utawala wa nasaba ya Qin Jamhuri ya China Jamhuri ya Watu wa China ilitangazwa |
1766 KK 221 KK 10 Oktoba 1911 1 Oktoba 1949 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
km² 9,596,961 km² (ya 33) 0.282 | ||||
Idadi ya watu - Januari 2020 kadirio - 2010 sensa - Msongamano wa watu |
1,400,000,0004 (ya 1) 1,339,724,852 145/km² (ya 83 (2)) | ||||
Fedha | Renminbi Yuan5, 2 (CNY )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC+8) not observed (UTC+8) | ||||
Intaneti TLD | .cn2 | ||||
Kodi ya simu | +862
- | ||||
1 Pamoja na Kimandarini kile cha Kikantoni ni lugha rasmi katika Hong Kong na Macau. Kiingereza ni pia lugha rasmi katika Hong Kong na Kireno huko Macau. Vilevile kuna lugha za kieneo yanayotumiwa rasmi kama vile Kiuyghur huko Xinjiang, Kimongolia katika jimbo la Mongolia ya Ndani, Kitibet huko Tibet na Kikorea katika mkoa wa Yanbian. |
China (pia: Uchina, Sina; kirefu: Jamhuri ya Watu wa China) ni nchi kubwa ya Asia ya Mashariki ambayo ndiyo nchi yenye watu wengi kuliko zote duniani.
China imepakana na Vietnam, Laos, Myanmar, India, Bhutan, Nepal, Pakistan, Afghanistan, Tajikistan, Kyrgyzstan, Kazakhstan, Urusi, Mongolia, Korea ya Kaskazini.
Kuna pwani ndefu kwenye Bahari ya Kusini ya China na Bahari ya Mashariki ya China ambazo ni bahari ya kando ya Pasifiki.
China kuna makabila 56 tofauti. Wahan ndio kabila kubwa zaidi nchini China kwa idadi ya watu ikiwa na asilimia 92.
Lugha rasmi ni Kichina cha Mandarin kinachotumiwa na asilimia 70 za wananchi.
Siasa inatawaliwa na chama cha kikomunisti.
Mji mkuu ni Beijing lakini Shanghai ndio mji mkubwa zaidi.
Hong Kong iliyokuwa koloni la Uingereza na Macau iliyokuwa koloni la Ureno ni maeneo ya China yenye utawala wa pekee.
Taiwan na visiwa vingine vya Jamhuri ya China vinatazamwa na serikali ya Beijing kuwa majimbo yake lakini vimekuwa kama nchi ya pekee tangu mwaka 1949.