| |||||
Kaulimbiu ya taifa: {{{national_motto}}} | |||||
Wimbo wa taifa: "Kimi Ga Yo (君が代)" (Utawala wa Kaisari) | |||||
Mji mkuu | Tokyo | ||||
Mji mkubwa nchini | marundiko ya Toko1 | ||||
Lugha rasmi | Kijapani (Nihongo) | ||||
Serikali | Ufalme wa kikatiba Naruhito (徳仁) Fumio Kishida (岸田 文雄) | ||||
Tarehe za Kihistoria Mwanzo wa Taifa Katiba ya Meiji Katiba ya Japani Mkataba wa San Francisco |
11 Februari, 660 BCE2 29 Novemba 1890 3 Mei 1947 28 Aprili 1952 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
377,944 km² (ya 62) 1.4% | ||||
Idadi ya watu - 2021 kadirio - 2020 sensa - Msongamano wa watu |
125,360,000 (ya 10) 126,226,568 334/km² (ya 36) | ||||
Fedha | Yen (¥) (JPY )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
JST (UTC+9) None (UTC) | ||||
Intaneti TLD | .jp | ||||
Kodi ya simu | +81
| ||||
1 Yokohama ni mji mkubwa kisheria, lakini marundiko ya Tokyo (pamoja na Yokohama na miji mingine) ni makubwa. 2 Mapokeo ya Kijaponi hudai taifa lilianzishwa siku hiyo na Tenno Jimmu anayesemekana alikuwa Kaisari wa kwanza wa nchi. |
Japani ni nchi ya visiwa katika Pasifiki, mkabala wa mwambao wa mashariki ya Asia. Wajapani wenyewe hutumia jina la "Nihon" au "Nippon" lenye maana ya "Mwanzo wa jua". Hivyo Japani huitwa pia "Nchi ya Macheo".
Nchi ina eneo la km² 377.944; na wakazi milioni 127; idadi hiyo imeanza kupungua.
Japani ni kati ya nchi za dunia zilizoendelea sana upande wa sayansi, teknolojia na uchumi. Ilikuwa nchi ya kwanza nje ya Ulaya iliyofaulu kujenga jamii ya viwanda.