Jeni

Picha halisi ya padri Gregor Mendel, baba wa jenetikia.

Jeni (pia kinasaba; kwa Kiingereza "gene", kutoka Kigiriki γόνος, gonos, yaani uzao) ni sehemu kwenye DNA. DNA ni mkusanyiko wa taarifa za kemikali ambazo hubeba maelekezo kwa ajili ya kutengeneza protini kwenye seli. Kila jeni au kinasaba hubeba habari zinazothibiti tabia za binadamu na kila kiumbehai (kama vile wanyama na mimea) zilizopokewa kutoka wazazi kama vile mwonekano, jinsia na maumbile yote.

Kila jeni ina seti moja ya maelekezo. Maelekezo hayo kawaida ni msimbo wa protini fulani.

DNA ya binadamu huwa na jeni takribani 27,000. Nusu ya jeni ya mtu hutoka kwa mama. Nusu nyingine hutoka kwa baba.


Developed by StudentB