Joto

Joto ni hali ya umotomoto wa mtu, kitu au sehemu fulani. Linapozidi huweza kusababisha kuungua kwa kitu kilichokabiliwa au kushika kitu chenye joto lililozidi.[1]

Pia ipo mikoa yenye joto kali (kama vile nchini Tanzania, Dar es Salaam, Pemba). Mikoa hii ipo karibu na bahari ya Hindi kwani wanasayansi huelezea zaidi kuhusu kisa cha mikoa hii kuwa na joto kali kadiri unaposogea karibu na usawa wa bahari ndivyo joto linavyoongezeka.

Pia kunapotokea msuguano baina ya vitu viwili huweza kuleta joto.

Mababu waliweza kupata joto kwa kukaa karibu na moto, hivyo hali hii huonesha kwamba moto huweza kusababisha joto na joto huweza kusababisha moto. Lakini moto si joto, wala joto si moto.

Joto lina umuhimu mkubwa kwa binadamu kwani joto la binadamu ni nyuzi joto 36.9 au 37, hivyo joto linapozidi au linapopungua huweza kumsababishia binadamu kufariki kwa kiasi cha joto lililopungua au kuongezeka endapo atakosa matibabu.

Pia joto hutumika katika uhifadhi wa chakula. Mfano wa vyakula vinavyoweza kuhifadhiwa ni mihogo, mahindi n.k. [2]

  1. Van Wylen, Gordon; Sonntag, Richard (1978). Fundamentals of Classical Thermodynamics (tol. la Second edition, SI Version, Revised Printing). Chapter 4.7, Definition of Heat: John Wiley & Sons. uk. 76. ISBN 0-471-04188-2.{{cite book}}: CS1 maint: location (link)
  2. D.V. Schroeder (1999). An Introduction to Thermal Physics. Addison-Wesley. uk. 15. ISBN 0-201-38027-7.

Developed by StudentB