Kamusi elezo

Encyclopedia Britannica ilikuwa kamusi elezo mashuhuri zaidi duniani hadi kuja kwa Wikipedia.

Kamusi elezo (pia: ensaiklopidia kutoka Kiingereza: encyclopedia) ni kitabu kinachokusudiwa kukusanya ujuzi wa binadamu kadiri iwezekanavyo kulingana na wingi wa kurasa zake.

Siku hizi, Wikipedia ni kamusi elezo kubwa zaidi duniani lakini si kitabu cha karatasi, ni mkusanyo wa habari kwa umbo dijitali katika intaneti. Zamani (kabla ya kuja kwa Wikipedia) Encyclopedia Britannica ilikuwa kati ya kamusi elezo kubwa zaidi iliyokuwa ikitolewa kama vitabu vilivyochapishwa.


Developed by StudentB