Karatasi

Laha ya karatasi.
Konge za ubao jinsi zinavyoonekana kwa hadubini ni chanzo cha karatasi.
Vikuto vya karatasi vyatumiwa kwenye mashine kubwa za kuchapa.

Karatasi (kutoka Kigiriki Χαρτί kharti kupitia Kiarabu قرطاص qartas) ni laha bapa na nyembamba ya konge za mimea zilizokandamizwa na kushikamanishwa. Watu huandika kwenye karatasi, vitabu na magazeti hufanywa kwa karatasi, tena vipande vikubwa vya karatasi hutumika kwa kufunga vitu ndani yake.

Karatasi hunywa kiowevu, hivyo hutumiwa pia kwa shughuli za kusafisha.

Karatasi hutengenezwa hasa kutokana na ubao uliosagwa lakini inawezekana kutumia konge za mimea mingine pia. Inawezekana kutumia pia karatasi iliyokwishatumiwa (kwa mfano magazeti ya kale) kwa kutengezea karatasi mpya.

Kwa matumizi mengine kuna pia karatasi nene kama bapa inayotumiwa kutengezea maboksi ya kubebea vifaa.

Watu wa kwanza kutengeneza karatasi walikuwa Wachina.


Developed by StudentB