Kitabu

Biblia mojawapo iliyochapwa na Gutenberg. Tangu hapo Biblia imekuwa kitabu kilichoenea zaidi.
Kamusi ya Kilatini.

Kitabu (kutoka Kiarabu كتاب, kitabun) ni mkusanyo wa kurasa zilizofungwa pamoja kwa njia ya kudumu. Siku hizi kitabu kimekuwa hasa mkusanyo wa kurasa za karatasi zilizochapishwa.

UNESCO imetoa elezo kuwa kitabu ni tangazo kwa umma lililochapishwa lenye kurasa zisizopungua 49.

Lakini kuna pia vitabu vyenye kurasa tupu vitakavyoandikwa kwa mkono.

Hadi karne ya 15 BK vitabu vyote viliandikwa kwa mkono kwa kutumia kalamu; kwa sababu hii vilikuwa vichache na bei ilikuwa juu.

Johannes Gutenberg alibuni mashine ya kuchapisha vitabu iliyofanikiwa na kurahisisha vitabu sana.

Siku hizi vitabu hutolewa pia kwa njia ya mtandao au CD kama vitabu pepe.

Kitabu kilichochapishwa mara nyingi zaidi duniani ni Biblia ya Kikristo: imetolewa katika nakala bilioni 5-6 hivi.


Developed by StudentB