Kitambaa (pia kitambara) ni kipande cha tambaa au jora ambalo kimekatwa ili kushonea vazi la binadamu, kama vile shati, sketi au suruali, au kwa madhumuni mengine, kama vile kutandika meza, kochi au samani nyingine, kushonea pazia, kurembesha, kupenga, kuosha, kupangusa vitu zilizomwagikiwa kiowevu na pia vitu vikavu kama vile madirisha ya glasi n.k.
Siku hizi vitambaa vinatengenezwa kwa kawaida katika viwanda. Mara nyingi hutengenezwa kwa kuunganisha nyuzi pamoja, ziwe za asili au vitu vilivyotengenezwa na mwanadamu. Mifano ya nyuzi za asili ni pamba na hariri. Mifano ya nyuzi zilizotengenezwa na binadamu ni nailoni na akriliki[1].
Rangi ya kitambaa inazingatiwa sana katika matumizi, kulingana na utamaduni, hali n.k.