Liturujia ya Roma ni liturujia iliyoenea katika sehemu kubwa ya Kanisa Katoliki, kutoka makao yake makuu, Roma (Italia).
Kwa asili yake ni liturujia ya Kilatini, ingawa kwa sasa inaadhimishwa katika lugha nyingi duniani kote.
Kilichochangia uenezi huo ni hasa heshima ya Kanisa la Roma na askofu wake, Papa.
Katika baadhi ya nchi, kama vile Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, baraza la maaskofu limekubaliwa kutamadunisha liturujia hiyo, bila ya kuvunja umoja wake wa msingi.