Jiji la Lusaka | |
Mahali pa mji wa Lusaka katika Zambia |
|
Majiranukta: 15°24′59″S 28°16′55″E / 15.41639°S 28.28194°E | |
Nchi | Zambia |
---|---|
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 1 300 000 |
Lusaka ni mji mkuu wa Zambia. Jiji la Lusaka liko Kusini ya Kati ya Zambia, na mahali pake ni 15°25' Kusini, 28°17' Mashariki [1] Archived 25 Machi 2011 at the Wayback Machine.. Iko futi 4200 (au mita 1400) juu ya UB. Idadi ya wakazi wake imekadiriwa kuwa watu 1,391,000 (mwaka wa 2000).
Mji wa Lusaka ulianzishwa mwaka wa 1905 na wakoloni Wazungu kwenye mahali pa kijiji ambacho mwenyekiti wake aliitwa Lusaaka. Kwa vile Lusaka iko katikati ya nchi, mwaka wa 1935 wakoloni Waingereza walihamishia mji mkuu wao wa Rhodesia ya Kaskazini huko kutoka mji wa Livingstone. Baada ya kupata uhuru, Lusaka ikaendelea kama mji mkuu wa Zambia hadi hivi sasa.
Lusaka hufikika kupitia kiwanja cha ndege cha kimataifa (Lusaka International Airport), au kupitia garimoshi kwenye njia ya reli inayoelekea kutoka mji wa Livingstone kwenda mji wa Kitwe.