Majimbo ya Ujerumani ni sehemu zinazounda Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani.
Tangu mwaka 1990 ambapo maeneo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kijerumani (1949 hadi 1990, ilijulikana pia kama Ujerumani wa Mashariki) yalijiunga na shirikisho kuna majimbo 16.
Majimbo hujitawala katika mambo mbalimbali kulingana na katiba ya Ujerumani.
Kila jimbo lina katiba yake, serikali, bunge na mahakama kulingana na mgawanyo wa madaraka.
Mabunge ya majimbo huchagua wawakilishi katika Bundesrat (Halmashauri ya Jamhuri ya Shirikisho) ambayo ni kitengo cha bunge la kitaifa pamoja na Bundestag.