Mazingira

Mazingira ya kiafrika

Mazingira ni jumla ya mambo yote yanayomzuguka kiumbe katika maisha yake. Kwa hiyo kila unachokiona ni mazingira yako.

Mazingira huweza kuundwa na vitu mbalimbali; yanaweza kuwa ya asili (kama misitu, milima, maziwa, mabonde, mito, bahari n.k.) au ya kutengenezwa na binadamu (kama majengo, viwanda n.k.).

Hivyo tunapaswa tuwe makini katika kujenga mazingira yetu kwa sababu vitu vingine huyaharibu, kama vile uchafuzi wa hewa, uchafuzi wa bahari, uchafuzi wa ardhi, n.k.

Tunapaswa kutunza mazingira yetu kwa sababu kilimo, ufugaji mvua, n.k. huathiriwa na uchafuzi wa mazingira. Mazingira hutunzwa kwa njia mbalimbali kama vile kupanda miti kwa wingi, kutunza vyanzo vyetu vya maji, na kutumia maji vizuri, hasa katika shughuli za kilimo, ili kuliepuka tatizo la ukame.


Developed by StudentB