Mia (kutoka neno la Kiarabu) ni namba inayoandikwa 100 (moja sifuri sifuri) kwa tarakimu za kawaida , ila kwa namba za Kirumi Ⅽ tu (kutokana na neno la Kilatini centum, yaani mia moja).
Ni namba asilia inayofuata 99 na kutangulia 101.
Vigawo vyake vya namba tasa ni: 2 x 2 x 5 x 5.
Ni mraba wa 10, hivyo inaweza kuandikwa 102.
Namba 100 ni msingi wa asilimia, 100% ikiwa kiwango kilichokamilika.