Michezo ya Afrika Nzima

Lagos 1973

Michezo ya Afrika Nzima (pia huitwa Michezo ya Afrika au Michezo ya Pan Afrika) ni tukio la michezo mbalimbali ya mataifa ya Afrika linalofanyika kila baada ya miaka minne, linaloandaliwa na Muungano wa Kamati za Kitaifa za Olimpiki za Afrika (ANOCA). Mataifa yote yanayoshiriki lazima yawe ya bara la Afrika.

Tukio la kwanza lilifanyika mwaka wa 1965 katika mji wa Brazzaville, nchini Jamhuri ya Kongo. Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) ilitoa utambulisho rasmi kwa tukio hilo kama tukio la bara la michezo mbalimbali, sambamba na michezo ya Pan American na Michezo ya Bara la Asia.


Developed by StudentB