Milele

Milele ni neno linalomaanisha uwepo usio na mwanzo wala mwisho unavyosadikiwa na dini mbalimbali kuhusu Mungu.

Wazo hilo gumu kufikiriwa linapingana na lile la muda ambalo linaeleweka kirahisi kwa sababu binadamu amezoea mfululizo wa nyakati, kama vile jana, leo na kesho.

Kama vile muda unavyoendana na mabadiliko, milele ni hali isiyokubali badiliko lolote, kutokana na ukamilifu wake.

Ni maarufu ufafanuzi wake uliotolewa na Severino Boesyo kwa Kilatini: "Interminabilis vitae tota simul et perfecta possessio" (Consolatio Philosophiae, V, vi). Tafsiri yake ni: "Uzima usio na mwisho unaomilikiwa wote pamoja na kikamilifu".


Developed by StudentB