Milki ya Bornu

Milki ya Bornu mnamo 1810.
Mahali pa Bornu kwenye ramani ya Kijerumani iliyochorwa mnamo 1891 (sehemu ya juu - kulia)

Bornu (pia Borno[1]) ilikuwa milki muhimu katika Afrika ya Magharibi kwenye ukanda wa Saheli katika maeneo ya nchi za leo Nigeria, Niger na Chadi.

Mnamo mwaka 1800 ilikuwa na uenezaji mkubwa na kumiliki eneo la takriban kilomita za mraba 242.701 pamoja na Ziwa Chad. Ilipakana wakati ule na Mandara, Emirati ya Adamawa, Ukhalifa wa Sokoto na maeneo ya Watuareg kwenye Sahara.

Bornu ilivamiwa mwaka 1893 na mfanyabiashara Mwarabu Rabih ben Fadlallah aliyeshinda na kuua watawala wake. Mwenyewe alivamiwa na Wafaransa waliopanua himaya yao barani Afrika wakati ule. Milki ya Bornu iligawiwa kati ya Ufaransa, Uingereza na Ujerumani.

Sehemu ya Kiingereza iliingizwa katika koloni la Nigeria na hapo kuendelea kwa jina kama milki chini ya "shehu" wa familia ya wafalme wa kale lakini chini ya usimamizi wa Waingereza. Milki hii inaendelea kwa jina katika jimbo la Nigeria linaloitwa Borno.

  1. Katika Wikipedia hii tunatumia "Bornu" kama jina la milki ya kihistoria na "Borno" kama jina la jimbo la Nigeria ingawa ni neno lilelile

Developed by StudentB