Mnururisho

Mnururisho (ing. radiation) ni uenezaji wa nishati kwa njia ya chembe ndogo sana au kwa njia ya mawimbi. Mnururisho huwa na chanzo, mwelekeo usionyoka na kasi.

Nuru inayoonekana kwa macho ni sehemu tu ya mnururisho wa sumakuumeme. Mawimbi ya nuru ni sehemu ya mawimbi mengine ya sumakuumeme

Mifano ya mnururisho inayoonekana au kusikika kirahisi ni nuru na joto. Binadamu ana milango ya fahamu kwa ajili mnurirsho huo kama vile macho kwa nuru na neva kenye ngozi kwa joto. Mifano ya mnururisho isiyoonekana ni mnururisho wa sumakuumeme katika redio na TV, eksirei au kinyuklia. Kuna viumbe vyenye milango ya fahamu kwa minururisho mingine, kwa mfano samaki au ndege zinazotambua uga za umeme au sumaku. Nyuki huona infraredi isiyoonekana kwa macho ya kibinadamu.


Developed by StudentB