Moto

Moto mkubwa.
Pembetatu ya moto inaonyesha masharti matatu yanayohitajika kwa moto kuwaka.
Kiberiti kinawaka.

Moto ni hali ya kuungua haraka kwa gimba na kutoa joto pamoja na nuru. Kisayansi ni mmenyuko wa kikemia kati ya oksijeni ya hewani na kampaundi za kaboni. Moto ni mfano mkuu wa harakati ya kuoksidisha.

Katika historia ya binadamu matumizi ya moto yalikuwa hatua kubwa ya kujenga utamaduni. Watu hutumia moto kwa kupika, kujilinda dhidi ya baridi na giza, kupeana habari, kuendesha vyombo vya usafiri na kutengeneza umeme.

Moto ni pia jambo haribifuː unaleta hatari kwa mali, afya na maisha ya watu na viumbe vyote.


Developed by StudentB