Kwa maana mengine ya neno hili tazama mpira (maana)
Mpira ni kifaa chenye umbo la tufe, duaradufu au umbo la kufanana nalo. Unatumiwa kwa kuutupa au kuupiga kwa mguu au fimbo fulani.
Mipira hutengenezwa kwa mata kama ngozi, plastiki au dutu ya mpira inayotakiwa kuwa nyumbufu. Mara nyingi mpira ni aina ya ganda tu inayojaa hewa lakini kuna pia mipira inayojaa dutu fulani kwa mfano mpira wa golf au hockey.
Michezo ya mipira inaaminiwa kuwa kati ya michezo ya kale kabisa. Maana inaonekana si watoto wadogo lakini pia wanyama kama paka huvutwa na kitu chenye mwendo wa kuzunguka.