| |||
Lugha ya taifa | Kireno | ||
Mji Mkuu | Maputo | ||
Aina ya Serikali | Jamhuri | ||
Rais | Filipe Nyusi | ||
Waziri Mkuu | Adriano Maleiane | ||
Eneo | km² 801.590 | ||
Wakazi | 31,693,239 (Julai 2022) | ||
Wakazi kwa km² | 28.7 | ||
JPT/ Mkazi | 233 US-$ (2004) | ||
Uhuru | kutoka Ureno tar. 25 June 1975 | ||
Pesa | Metical (MZM) | ||
Wakati | UTC +2h | ||
Wimbo wa Taifa | Pátria Amada (kwa Kireno: Nchi pendwa) | ||
Namba ya simu ya kimataifa | +258 | ||
Msumbiji (kwa Kireno: Moçambique) ni nchi ya Afrika ya Kusini-Mashariki.
Msumbiji iko ufukoni mwa Bahari Hindi ikipakana na Tanzania, Malawi, Zambia, Zimbabwe, Afrika Kusini na Eswatini.
Upande wa mashariki kuna kisiwa cha Madagaska ng'ambo ya mlango bahari wa Msumbiji.
Jina la nchi limetokana na Kisiwa cha Msumbiji (kwa Kireno: Ilha de Moçambique) kilichokuwa boma na makao makuu ya Ureno kwenye pwani ya Afrika ya Mashariki.
Sikukuu ya Taifa ni tarehe 25 Juni, ulipopatikana na uhuru mwaka 1975.