Mwana wa Adamu

Mwana wa Adamu akiwa na upanga kati ya vinara saba, kadiri ya Ufunuo wa Yohane; mchoro mdogo wa karne ya 11 kutoka Bamberg.

Mwana wa Adamu (kwa Kiebrania בן–אדם, ben-'adam, yaani binadamu; kwa Kigiriki "ὁ υἱὸς τοὺ ἀνθρώπου", ho huios tou anthropou, "mwana wa mtu") ni jina lililotumiwa na Yesu Kristo katika kujitaja ili kujitambulisha. Limeandikwa mara nyingi katika Injili, Matendo ya Mitume na Kitabu cha Ufunuo, ingawa halikuendelea kutumiwa sana na Wakristo waliopendelea jina "Mwana wa Mungu".[1][2][3]

Mara 81 linapatikana katika Injili, lakini daima mdomoni mwa Yesu.[4] Inawezekana mwenyewe alilipenda kwa sababu Wayahudi walikuwa hawalitumii kwa kulipotosha kama ilivyokuwa kwa jina Masiya walilolielewa kisiasa.

Pia jina hilo liliweza kudokeza unyonge wa kibinadamu ambao Mwana aliutwaa, pamoja na utukufu wake ujao, kadiri ya kitabu cha Danieli (7:13-14).

  1. Jesus and the Son of Man by A J B Higgins 2002 ISBN 0-227-17221-3 pages 13-15
  2. Jesus Remembered: Christianity in the Making by James D. G. Dunn (Jul 29, 2003) ISBN 0802839312 pages 724-725
  3. The Son of Man Debate: A History and Evaluation by Delbert Royce Burkett (Jan 28, 2000) Cambridge Univ Press ISBN 0521663067 pages 3-5
  4. Lord Jesus Christ: Devotion to Jesus in Earliest Christianity by Larry W. Hurtado, ISBN 0-8028-3167-2 Wm B. Eerdmans Publishing Co., 2005 pages 290-293

Developed by StudentB