Ndege (Aves) | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Ndege (Buabua-kishungi mkubwa)
| ||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
| ||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||
Nusungeli na oda za juu: |
Ndege ni wanyama wenye uti wa mgongo (chordata) na miguu miwili wanaozaliana kwa kutaga mayai.
Biolojia inawapanga katika ngeli ya Aves.
Ndege wameenea kote duniani kuanzia Aktiki hadi Antaktiki.
Ndege mdogo huwa na sentimita 5 tu na ndege mkubwa ana urefu wa mita mbili na nusu.
Ndege huwa na manyoya, mdomo bila meno, mayai yenye ganda gumu, moyo wenye vyumba vinne na mifupa myepesi ambayo ni imara.
Ndege walio wengi wana uwezo wa kuruka hewani na maumbile yao yanalingana na kusafiri hewani. Ila tu aina chache zimepoteza uwezo wa kuruka kwa mfano mbuni, ngwini na ndege kadhaa wa visiwani.
Aina nyingi za ndege huwa na misafara ya kila mwaka, kwa mfano korongo mweupe husafiri kila mwaka kati ya Afrika na Ulaya.