Nukta

Kwa nukta kama kipimo cha wakati angalia sekunde

Picha iliyochorwa kwa kutumia nukta tu.
(Kama nukta inachorwa inaonekana kama duara ndogo)

Nukta (kutoka Kiarabu نقطة, nuqta; kwa Kiingereza: point) katika elimu ya hisabati na jiografia ni kitu au mahali bila urefu wala upana, yaani bila eneo lolote.

Nukta haina pande wala haiwezi kugawiwa.

Kwa lugha ya jiometria inaweza kuelezwa pia kuwa duara yenye kipenyo cha 0.

Lakini ina mahali panapoweza kutajwa.


Developed by StudentB