Nyama ni sehemu za mwili wa wanyama zinazoliwa kama chakula au kitoweo.
Kwa watu wengi nyama ni chakula muhimu kwa sababu ina protini nyingi ndani yake pamoja na mafuta. Nyama huliwa baada ya kuipika, kuchoma au kukaanga. Kuna sehemu za dunia ambako watu wamezoea kula nyama mbichi wakiteua sehemu lainilaini, kwa mfano nyama ya kusagwa au maini.