Papa Pius IX

Mwenye heri Pius IX.

Papa Pius IX (13 Mei 17927 Februari 1878) alikuwa Papa kuanzia tarehe 16/21 Juni 1846 hadi kifo chake[1]. Alitokea Senigallia, Italia[2].

Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Giovanni Maria Mastai-Ferretti.

Alimfuata Papa Gregori XVI akafuatwa na Papa Leo XIII.

Upapa wake ulidumu kuliko ule wa mwingine yeyote ya historia ya Kanisa, ukichukua zaidi ya miaka 31.

Wakati huo aliitisha Mtaguso II wa Vatikano (18691870), uliotangaza dogma ya kwamba Papa ana karama ya kutodanganyika anapofundisha katika nafasi za pekee.

Pamoja na hayo, mtaguso huo ulikatika kutokana na jeshi la Italia kuteka Roma. Hivyo alikuwa wa mwisho kutawala Dola la Papa na wa kwanza kujifungia ndani ya Vatikano ili kupinga uvamizi huo.

Kabla ya hapo, tarehe 8 Desemba 1854 Pius IX alikuwa ametangaza dogma ya Bikira Maria Kukingiwa Dhambi ya Asili. Pia aliandika nyaraka 38 kuhusu masuala mbalimbali.

Alitangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa mwenye heri tarehe 3 Septemba 2000.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[3].

  1. https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
  2. https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
  3. Martyrologium Romanum

Developed by StudentB